Sevilla FC Kutua Nchini Kuumana Na Simba SC Na Kiingilio Ni Buku Tano Tu

DAR ES SALAAM, Tanzania -Kampuni ya SportPesa kwa kushirikiana na Ligi Bora duniani ya LaLiga tunaileta nchini klabu ya Sevilla FC.

Ziara hiyo inayokwenda kwa jina la ‘LaLiga World SportPesa Challenge” itawashuhudia mabingwa hao mara tano wa UEFA Europa League wakiumana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba SC, siku ya Alhamisi ya Mei 23 katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 Usiku

Kwa kiingilio cha Tsh 5000/= tu, wapenzi wa soka nchini watapata kushuhudia mastaa wa Sevilla kama vile Jesus Navas, Wissam Ben Yedder, Pablo Sarabia na wengine wengi wakitandaza kandanda safi dhidi ya nyota wa Simba.

Mbali na kiingilio cha Tsh 5000/= kwa upande wa mzunguko, Shirikisho la Soka nchini (TFF) limetangaza bei nyingine za tiketi kuwa ni Tsh 15,000/= kwa jukwaa la VIP ‘B’ na Tsh 100,000/= kwa watu wa Platinum ambao watapewa usafiri wa kwenda uwanjani, vinywaji na chakula wakiwa uwanjani pamoja na jezi.

Sambamba na mechi hiyo ya kukata na shoka, jopo zima la Sevilla litatembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini, kufanya semina elekezi kwa viongozi wa soka nchini pamoja na kliniki za soka kwa wachezaji na makocha.

Rekodi ya Kimataifa

Simba wameithibitishia Tanzania na Afrika kwa ujumla kuwa moja ya timu ngumu kufungika kwenye uwanja wake wa nyumbani katika michezo saba ya kimataifa iliyocheza msimu huu.

Wekundu hao wa Msimbazi wametoa dozi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Mbabane Swallows (Swaziland), Nkana FC (Zambia), JS Soura (Algeria), Al Ahly (Misri ) bila kusahau ule ushindi maarufu dhidi ya AS Vita kutoka Jamhuri ya Congo uliowapa tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali huku wakienda sare ya 0-0 na TP Mazembe kwenye hatua ya robo fainali.

Tanzania itafaidika vipi?

Ziara hii ya kimichezo nchini inatarajiwa kuitangaza Tanzania kimataifa kama moja ya sehemu bora kwa timu kubwa za Ulaya kutembelea baada ya msimu au kabla kuanza kwa msimu mpya.

Si tu hivyo, bali wadau wa soka nchini kama vile viongozi wa TFF na Vilabu, makocha na wachezaji watapata nafasi ya kujifunza mbinu za kisasa za uendeshaji soka nje na ndani ya uwanja.

Ujio wa Sevilla pia unatarajiwa kuwa fursa pekee kuvitangaza vivutio vyetu vya Utalii nchini bila kusahau utamaduni wetu uliotukuka.

Sevilla itakuwa timu ya kwanza kutoka LaLiga na timu ya pili kutoka barani Ulaya kutembelea Tanzania kwa udhamini wa SportPesa baada ya Everton kufanya hivyo Julai 2017 ambapo wapenzi wa soka nchini walipata nafasi ya kumshuhudia Wayne Rooney akiichezea Everton mechi yake ya kwanza baada ya miaka 13 kupita.

Unaweza kununua tiketi yako sasa kupitia App ya Selcom ukiwa mahali popote au tembelea vituo vya mafuta vya Puma jijini Dar es Salaam.

Lakini pia usisahau kutembelea kurasa zetu za kijamii za Facebook, Twitter au Instagram ambapo pia unaweza kujishindia tiketi ya mechi.

Je, Sevilla itakuwa timu ya kwanza ya kimataifa kuifunga Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam msimu huu?

Mkeka

Namba za Malipo

  • 150888
  • 150888
  • 150888
  • 150888
  • 150888

Huduma kwa Wateja

Tunatoa huduma angalifu kwa wateja masaa 24 kwa wachezaji wa SportPesa.